Korea Kaskazini yasema vikwazo vitawasaidia

Pyongyang, Korea Kaskazini.  Viongozi wa Marekani na China walikubaliana jana ‘kuzidisha mbinyo’ dhidi ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, lakini naye aliwajibu kwamba vikwazo zaidi vitaisaidia kuharakisha programu yake ya ukamilishaji silaha za nyuklia.
"Ongezeko la hatu ya Marekani na washirika wake kuiwekewa vikwazo na mbinyo zaidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea Kaskazini (DPRK) itatuongezea kasi kuelekea kukamilisha mkakati wa kuwa taifa la nyuklia,’ ilisema taarifa ya Korea Kaskazini kwa vyombo vya habari jana.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini kutokana na kufanya majaribio ya makombora na nyuklia likilenga kudhibiti vyanzo vya mapato vya nchi hiyo.
Vikwazo vipya vinahusu kupigwa marufuku uuzaji nchi za nje bidhaa za nguo, kuwanyima vibali vya kufanya kazi wafanyakazi kutoka Korea Kaskazini na kupunguza kiasi cha mafuta.
Vikwazo hivyo vipya vimekuja mwezi mmoja tangu Korea Kaskazini iwekewe vikwazo vingine lengo likiwa sasa kuikosesha mapato ya dola za Marekani bilioni moja kutoka dola bilioni tatu za mapato yam waka yanayotokana na kodi.

Comments