MASTAA WALIOLIPWA PESA NYINGI ZAIDI DUNIANI MWAKA 2017

Kwa mujibu wa  jarida maarufu duniani la Forbes, miezi 12 iliyopita, mastaa 100 wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani waliingiza jumla ya Tsh trioni 11 ikiwa fedha nyingi kuliko pato la taifa la nchi tatu za Bekize, Liberia na Gambia zikichanganywa kwa pamoja.
Katika orodha hiyo ya mastaa 100 walioingiza fedha nyingi, inaongozwa na mwanamuziki kutoka nchini marekani, Diddy ambaye pekee aliingiza jumla ya Tsh 291 bilioni ambapo anafwatiwa na mwanamuziki wa kike Beyonce na J.K Rownling ambao wanahitimisha tatu bora ya mastaa wenye mkwanja mrefu.
Orodha hiyo ya  mastaa 100 imejumuisha watu kutoka tasnia mbalimbali kama vile utangazaji, yanamuziki, michezo mbalimbali lakini wanamuziki hasa kutoka nchini marekani wanaonekana kutawala katika mastaa 10 wa mwanzo.
Orodha hii imejumuisha kipato kilicho ingizwa na mastaa husika kutoka Juni 1, 2016 hadi Juni 1, 2017. Fedha hizo ni kabla makato ya wanasheria, mameneja na mawakala wa mastaa hao.
Hapa chini tumeorodhesha mastaa 10 walioingiza mkwanja mrefu zaidi ikifuatiwa na fedha aliyoingiza na tasnia anayofanyia kazi pamoja na nchi atokayo staa huyo.
1.Diddy- $130milioni (Tsh bilioni 291), Mwanamuziki nchini Marekani
  1. Beyonce-$105milioi (Tsh billion 235), Mwanamuziki nchini Marekani
  2. J.K Rowling- $95milioni (Tsh bilioni 213), Mwanamuziki nchini Uingereza
  3. Drake-$94 milioni (Tsh bilioni210), Mwanamuzi nchini Marekani
  4. Cristiano Ronaldo -$93milioni (Billioni 208), Mchezaji nchini Ureno
  5. The Weekend-$92millioni (Tsh bilioni 206), mwanamuziki nchini Canada
  6. Howard Stern -$90milioni (Tsh bilioni 203) Mtangazaji nchini Marekani
  7. Coldplay-$88millioni (Tshbilioni 196) Mwanamuziki nchini Uingereza
  8. James Patterson -$87 milioni(Tsh billioni195) Mwanamuzi Nchini Marekani
  9. Lebron James- $86milioni (Tsh bilioni 192), Mchezaji nchini Marekani.
Unaweza kuiona orodha yote kwa kutembelea tovuti ya Forbes ambayo niwww.forbes.com

Comments