![]() |
| Angela Merkel na Emmanuel Macron mjini Tallinn, tarehe 28 Septemba 2017, kabla ya mkutano kuhusu masuala ya kidijitali. JANEK SKARZYNSKI / AFP |
Baada ya hotuba ya Emmanuel Macron kuhusu Ulaya na kuchaguliwa kwa mara nyingine kwa Angela Merkel, lengo lilikuwa ni kutoa sura yenye nguvu ya ushirikiano na kila mmoja kutoa maoni yake kuhusu mipango ya Ulaya.
Mkutano wa viongozi hawa unaonyesha picha nzuri ya kuungana lichamatatizo mbalimbali yanayoonyesha nia ya kuendeleza pamoja juu ya masuala ya Ulaya.
"Makubaliano makubwa" yapo, kwa mujibu wa Angela Merkel. Kansela wa Ujerumani anaoneaka kuridhika na maono ya Emmanuel Macron kuhusu Umoja wa Ulaya, huku akisema kuwa Ufaransa imeanza kujikita kuhusu maendeleo ya Ulaya
Ulinzi na uhamiaji ni masuala mawili ambayo washirika wanaweza kusonga mbele haraka. Kwa upande mwingine, suala la serikali ya kiuchumi ya eneo la nchi zinazotumia sarafu ya Euro linaloendekezwa na Ufaransa halikujadiliwa kwa undani.
Mazungumzo haya yamesaidia kuweka sawa mambo mengi kati ya viongozi hawa wawili. Hakuna hatua iliyojadiliwa kwa undani. Kansela wa Ujerumani bado anasubiri kuundwa kwa serikali mpya ya umoja ili kuongoza Ujerumani.
Lakini kutoa ushawishi mpya kwa Umoja wa Ulaya ni suala ambalo Angela Merkel anahitaji kabla ya mazungumzo ya moja kwa moja.

.
ReplyDelete