Orodha ya viongozi wa ACT Wazalendo waliohamia CCM

Siku ya leo, aliyekuwa Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo, Samson Mwigamba ametangaza kujivua uanachama wa chama chake na kuhamia Chama cha mapinduzi (CCM) ikiwa ni siku chache tu tokea alipoandika barua ya kujiuzulu nafasi ya uongozi wa chama hicho.

Mwigamba ametangaza uamuzi huo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kutangaza kwamba hakuondoka peke yake bali kuna kundi ambalo nalo limechukizwa na mwenendo wa chama cha ACT Wazalendo hivyo kuamua kujiunga CCM.

Alilitaja kundi hilo ambalo linahusisha viongozi na waliowahi kuwa viongozi wa chama hicho kuwa ni pamoja na

Wilson Laizer – Katibu mkoa wa Arusha
Nkamia John – Mwenyekiti wa jimbo la Singida
Wilfred Kitundu – Aliyekuwa mwenyekiti Mkoa wa Singida
Emmanuel Wilfred – Afisa Tawala wa
Lipuloth Robert – Katibu Mkoa wa Singida
Dansen doroth – Alikuwa Katibu Mkoa wa Arusha
Peter Mwambuja – Mhazini
Mwantumu Mgonja – Mwanasheria
Denis Chembu – Alikuwa Katibu wa Sheria
Mwigamba alitaja sababu za kujiondoa katika chama cha ACT Wazalendo kuwa ni pamoja na kukiukwa kwa misingi iliyochochea kuundwa kwa chama hicho, kutokuwepo kwa maelewano baina ya viongozi wa chama, pamoja na kuvutiwa na utendaji wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Comments